Wakizungumza wakati wa kupokea misaada hiyo waathirika wa mafuriko
hayo wamewashukuru kampuni ya Alsaid pamoja na wabunge akiwemo mbunge wa
viti maalumu mkoa wa Morogoro Devota Minja kwa jitihada zao walizo
zionyesha toka kutokea kwa mafuriko hayo huku wakiomba serikali
kuwasaidia kwa mambo mengine kama Mahema,vyandarua, pamoja na dawa kwa
kujikinga na magonjwa ya milipuko.
Kwaupande wake mkurugenzi wa kampuni ya mabasi ya ALSAID Mbaraka
Alsaed amesema kampuni yake itaendele kuwasaidia wahanga hao huku
akiziomba taasisi mbalimbali na mashirika kuwasaidia wahanga hao ilinao
waweze kuishi hasa katika kipindi hiki kigumu kwao.
Nao wabunge akiwemo mbunge wa jimbo la kilosa Mbaraka Bawaziri
ameshukuru misaada mbalimbali inayo endelea kutolewa na wahisani huku
mbunge viti maalumu mkoa wa morogoro devota minja akisema ipo haja ya
serikali kuangalia swala la ujenzi wa tuta la mto mkondoa ili
lisiendelee kesababisha hasara kwa watanzania na serikali.
Download Video and Put Comment
Toa Maoni Hapa Chini