Kampeni
za kukabiliana na ugonjwa wa Kipindupindu mkoani Arusha sasa
zitaanza kufanyika nyumba kwa nyumba hatua inayolenga kudhibiti
kuzagaa kwa maji machafu yakiwemo yanayotoka kwenye vyoo
vilivyojaa na mitaro iliyoziba.
Akizungumzia hatua iliyofikiwa kukabiliana na ugonjwa huo mkuu
wa mkoa wa Arusha Bw.Daud Felexs Ntebenda amesema licha ya kuwepo kwa
dalili nzuri za kuudhibiti ugonjwa huo ameagiza watu wote
wanaotiririsha maji machafu kukamatwa na kuchukuliwa hatua.
Kwa upande wao wananchi wa maeneo mbalimbali ya mkoa wa Arusha
wamesema jamii haijashirikishwa ipasavyo kukabiliana na janga la
Kipindupindu na wametaka serikali kuzishirikisha taasisi na mashirika
yakiwemo binafsi kukabiliana na janga hilo.
Arusha ni miongoni mwa mikoa inayokabiliwa na tatizo kubwa la
ukosefu wa miundombinu ya uondoaji wa majitaka ambalo licha ya
kuwepo kwa jitihada za kulikabili zinasuasua kutokana na ujenzi holela.
Download Video and Put Comment
Toa Maoni Hapa Chini