Anakwenda Ulaya na hiyo itakuwa safari
yake ya kwanza akiwa na Yanga itakayokwenda kuweka kambi yake nchini
Uturuki kujiandaa na mechi ya MO Bejaia ya Algeria na Mazembe.
Yanga inaondoka kesho Jumapili kwenda
Uturuki na haitaonekana tena hadi Juni 28, mwaka huu itapovaana na
wapinzani wao TP Mazembe.
Safari hiyo, itawajumuisha wachezaji
wengine wapya Juma Mahadh, Vincent Andrew ‘Dante’ na Beno Kakolanya
ambao hiyo itakuwa safari yao ya kwanza tangu watue kuichezea Yanga.
Kwa mujibu wa chanzo cha habari kutoka
ndani ya uongozi wa Yanga, timu hiyo kabla ya kwenda Algeria kuvaana na
MO Bejaia, kwanza itatua Uturuki kwa ajili ya kambi ya muda mfupi na
baadaye kuondoka.
Chanzo hicho kilisema, Yanga mara baada
ya mechi na MO Bejaia itakayopigwa wikiendi ijayo, watarejea tena
Uturuki na kupiga kambi ya siku tisa kuanzia Juni 20 hadi 26
watakapofika jijini Dar es Salaam siku mbili kabla ya mechi na Mazembe.
“Timu inaondoka keshokutwa (kesho
Jumapili), lakini haitaenda moja kwa moja Algeria badala yake tutaweka
kambi ya siku chache nchini Uturuki na baadaye tutaelekea Algeria kwa
ajili ya mechi na MO Bejaia.
“Mara baada ya mechi na MO Bejaia, timu
itarejea tena Uturuki kwa ajili ya kambi ndefu kidogo ya siku kama tisa
kuanzia Juni 20 hadi 26 na timu itarejea Dar siku mbili kabla ya mechi
na Mazembe tutakayoicheza Juni 28,” kilisema chanzo hicho.
Hata hivyo, Yanga inaondoka bila ya
nahodha wake Nadir Haroub ‘Cannavaro’ na Juma Abdul. Cannavaro
anatumikia adhabu ya kadi nyekundu aliyopewa katika mechi ya Kombe la
Shirikisho dhidi ya Sagrada Esperanca wakati Abdul ana maumivu ya enka.
Download Video and Put Comment
Toa Maoni Hapa Chini