Vijana
wa mkoa wa Geita wametakiwa kufanya kazi kwa bidii ili kujiletea
maendeleo yao binafsi na taifa kwa ujumla ili kujiondoa katika dimbwi la
umasikini ambapo takwimu zinaonyesha kuwa pamoja na mkoa huo kuwa na
rasilimali nyingi bado utajiri huo wa madini haujaweza kuwakomboa.
Katika kuhakikisha kila mtu anainuka kiuchumi ni lazima umoja na
mshikamano wa kazi uwepo kati ya jamii na serikali ambapo wananchi
wametakiwa kufanya kazi kwa kufuata sheria na taratibu za nchi huku
wananchi wakiiomba serikali kuhakikisha inawaboreshea miundombinu hasa
katika sekta ya madini.
Baadhi ya wananchi wa kijiji cha Nyakabale kilichopo jirani na
mgodi wa dhahabu wa Geita wakiongea mbele ya naibu waziri wa mambo ya
ndani wamelilalamikia jeshi la polisi kwa kila wanachokiita uvunjifu wa
haki za binadamu pale wanakijiji wanapokuwa katika shughuli zao za
kujipatia kipato jirani na mpaka wa mgodi huo.
Naye naibu waziri wa mambo ya ndani nchi Ahmad Masauni amesema
wizara yake itafuatilia malalamiko yote yaliyotolewa na wananchi pamoja
na wabunge wao juu ya ukiukwaji wa haki za binaadamu unaofanywa na
askari polisi wakishirikiana na wawekezaji, ili kubaini ukweli na sheria
ifuate mkondo.
Download Video and Put Comment
Toa Maoni Hapa Chini