Wanafunzi
wa shule ya Msingi Kakola iliyoko katika Halmashauri ya Msalala
wilayani Kahama Shinyanga wako hatarini kupatwa na magonjwa ya tumbo na
kipindupindu kufuatia vyoo vichache vya shule hiyo kufurika hali ambayo
inadaiwa kusababisshwa na baadhi ya viongozi wa kata na kijiji
kubadilisha matumizi ya fedha za ujenzi wa choo cha shule hiyo
zilizotolewa na Halmashauri ya Msalala.
Wakizungumzia hali hiyo baadhi ya wakazi wa kijiji cha kakola
wamewalalamikia baadhi ya viongozi wa kata na kijiji kuficha baadhi ya
nyaraka za miradi ya maendeleo na kutowasomea taarifa ya mapato na
matumizi huku wakimtaka mwenyekiti wa kijiji na diwani wa kata hiyo
Bw.John Shiganga kutamka hadharani ni lini choo cha shule hiyo
kitajengwa na kukamilika.
Akijibu tuhuma hizo kwa niaba ya diwani anayelalamikiwa kubadilisha
matumizi ya fedha za ujenzi wa choo cha shule ya Kakola mtendaji wa
kijiji hicho ambaye naye anadaiwa kushirikiana na diwani kukiuka
makubaliano Bw.Ramadhani Madefe amedai amesema alichotekikeleza ni
maagizo aliyopewa huku mwenyekiti wa kijiji cha kakola Bw.Emmanuel
Bombeda akilazimika kuwatuliza wananchi waliopatwa na hasira baada kuona
diwani wao hakufika katika mkutano huo kujimbu malalamiko yao.
Download Video and Put Comment
Toa Maoni Hapa Chini