Kikosi cha Serengeti Boys kikisherehekea kushika nafasi ya tatu kwenye mashindano ya mwaliko nchini India mwezi uliopita.
Nahodha
wa Timu ya Taifa ya vijana ya Tanzania chini ya umri wa miaka 17
Serengeti Boys, Issa Abdi amesema mashindano ya vijana yaliyofanyika
nchini India mwezi uliopita, yamewajenga vizuri, baada ya kukutana na
mataifa yaliyondelea kisoka kama Marekani na Korea Kusini.
Abdi amesema wanataraji kambi ya Juni 13 mwaka huu kujiandaa kufuzu fainali za Africa mwakani dhidi ya Shelisheli baadae mwezi huu, itakuwa ya kufanyia kazi mapungufu waliyobaini nchini India.
Aidha kwa upande mwengine, Nahodha huyo anayecheza nafasi ya kiungo, aliyeibuliwa kwenye mashindano ya Copa Coca Cola mwaka juzi, amesema wameona tofauti ya watoto wa mataifa yaliyoendelea kisoka wanaandaliwa tangu chini, tofauti na wao kutoka nchi zinazoendelea, wanafanya jitihada zao binafsi kukuza vipaji vyao.

Download Video and Put Comment
Toa Maoni Hapa Chini