Halmashauri
ya wilaya ya Karagwe imewaondoa kwenye mpango wa kunusuru kaya masikini
unaotekelezwa na mfuko wa maendeleo ya jamii(Tasaf III)walengwa
164,kutokana na walengwa hao kubainika kutokidhi vigezo vya mfuko huo.
Walengwa hao ambao awali walikuwa wakipokea ruzuku inayotolewa na
mfuko huo,wameondolewa mara baada ya uhakiki wa walengwa halali
wanaopaswa kupokea ruzuku hiyo,uliofanywa na wataalamu wa idara
mbalimbali kutoka ofisi ya mkurugenzi wa halmashauri hiyo.
Akiongea ITV Afisa Mshauri na Mfuatiliaji wa Tasaf wilaya ya
Karagwe Elias Sowani,idadi hiyo ya walengwa waliondolewa kwenye mpango
imetokana baada ya uhakiki wa kina,na kufanikiwa kubaini baadhi ya
walengwa hawakuwa na sifa zinazotambuliwa na mfuko huo,huku wengine
wakiwa na kasoro za kutokuwa raia wa nchi ya Tanzania.
Sowani amesema kuwa wengine walibainika kuwa ni wajumbe wa Serikali
za vijiji vyao,huku baadhi yao wakitolewa moja kwa moja kwenye orodha
kutokana na sababu za vifo.
Download Video and Put Comment
Toa Maoni Hapa Chini