Zaidi
ya watu miatatu wakazi wa kijiji cha Mlangarini wilaya ya Arumeru
wakiwa na mashoka jembe nyundo na mafekeo wamevamia zaidi ya hekari
mianne za shamba la mwekezaji kugawana kupanda mahindi na kutenga maeneo
ya huduma muhimu wakidai shamba ilo limekaa muda mrefu bila kutumika
huku wananchi wakikosa maeneo ya kilimo na huduma.
ITV ilifika katika kijiji cha Mlangarini na kushuhudia mamia ya
watu wakiwa na zana za jadi wakifeka kulima na kupanda mahindi kwenye
maeneo waliyo jigawia huku wakiahinisha maeneo ya huduma muhimu na kudai
wananchi wanateseka huku watu wachache wakimiliki maeneo makubwa bila
kuyatumia hivyo wameamua kugawana.
Wanawake kutoka katika kijiji hicho wameeleza namna wanavyo teseka
kwa kukodishwa mashamba hayo kwa ghalama ya juu na mashariti magumu na
kwamba wamefikisha kero hiyo ngazi mbalimbali bila mafanikio.
Wazee wanao kadiliwa kuwa na umri wa miaka sabini nawo wakatoa
historia fupi ya mashamba hayo huku wakiunga mkono hatua hiyo na katika
tukio ilo hapakuwepo kiongozi yoyote wa serikali na juhudi za kuwatafuta
viongozi wa wilaya ya Arumeru pamoja na mwekezaji zinaendelea.
Download Video and Put Comment
Toa Maoni Hapa Chini