Waziri wa afya Waziri wa Afya, Maendeleo ya Jamii, Jinsia, Wazee na
Watoto, Mh. Ummy Mwalimu amesema hayo bungeni mkoani Dodoma wakati
akiwasilisha bajeti ya wizara yake kwa mwaka wa fedha 2016/17 na
kuongeza kuwa katika bajeti ya safari hii wamedhamiria kuyatua matatizo
yote sugu yanayokabili sekta ya afya.
Kwa upande wake mwenyekiti wa kamati ya bunge ya huduma za jamii
kupitia mwenyekiti wake Peter Serukamba pamoja na kambi rasmi ya
upinzani bungeni kupitia msemaji wake Dr.Godwin Mollel wamesema hali ya
upatikanaji wa huduma za afya ni mbaya na ni bora Serikali ikaangalie
namna ya kuiboresha hasa maeneo ya vijijini.
Baadhi ya wabunge wakichangia bajeti ya wizara hiyo wamesema
hospitali kuhudumiwa na wizara mbili tofauti ya afya na Tamisemi
kunasababisha huduma kuzidi kulegalega kwa kile kinachoonekana wizara
hizo kutegeana.
Download Video and Put Comment
Toa Maoni Hapa Chini