Akiongea baada ya kufanya ukaguzi kwa wateja ambao wamekuwa
wakihujumu miundombinu ya Tanesco kwa niaba ya Meneja wa Tanesco mkoa wa
Singida,Afisa usalama wa shirika hilo Bwana Jumama Mahuba amesema
wamesha wakamata watu saba na watu wa tatu wamesha hukumiwa kifungo cha
miaka nane.
Katika hatua nyingine Bwana Mahuba amesema uharibifu wa miundo
mbinu ya Tanesco unao fanywa na baadhi ya watu itakuwa inavunja kasi ya
mheshiwa Rais ya kutata nchi kuwa ya viwanda,pia shirika limeomba watu
wanao wafahamu wanaohujumu miundombinu ya Tanesco kutoa taarifa na
watazawadiwa.
Akifanyiwa ukaguzi Bwana Emmanuel Yona makazi wa Isuna B wilayaya
Ikungi ambaye anadaiwa kuhujumu miundo mbinu ya Tanesco,amekiri
kujiunganishia umeme kwa kukwepesha katika mita kwenye nyumba zake
mbili tokea mwezi wa tisa mwaka jana.
Download Video and Put Comment
Toa Maoni Hapa Chini