Watu
watano wamefariki dunia kati yao watatu wakiwa wa familia moja baada
ya nyumba waliyokuwa wakiishi kufunikwa na udongo baada ya mvua kubwa
kunyesha kwa saa kumi wilayani Rungwe.
Mvua kubwa ambayo imenyesha kwa zaidi ya saa 10 mfululizo ndiyo
ambayo imesababisha udongo kuporomoka kutoka katika Mlima Mkomelo na
kusababisha madhara makubwa ikiwemo vifo vya watu watano na uharibifu wa
mazao ya chakula na biashara katika kijiji cha kitali,halmashauri ya
busokelo wilayani rungwe
Kutokana na maporomoko hayo ya udongo,familia ya Iman John Mwakyusa
imejikuta ikipoteza watoto watatu ambao ni wanafunzi baada ya nyumba
waliokuwa wakiishi kufunikwa na udongo.
Mratibu wa Maafa katika Halmashauri ya Busokelo Maombi John Msuta
amesema maafa hayo yametokana na mvua kubwa ambazo zinanyesha kwenye
eneo hilo na sasa halmashauri yake imeanza kuchukua hatua za tahadhari
ikiwemo kuwahamisha watu wanaoishi kwenye maeneo hatarishi.
Download Video and Put Comment
Toa Maoni Hapa Chini