TRA yagawa Zaidi ya mifuko 5000 ya sukari za magendo baada ya wenye mali kushindwa kulipa faini mkoani Lindi. | nyula blog

Habari Kila Pande

Breaking News
Loading...

Sunday, May 8, 2016

TRA yagawa Zaidi ya mifuko 5000 ya sukari za magendo baada ya wenye mali kushindwa kulipa faini mkoani Lindi.

Mamlaka ya Mapato Tanzania TRA mkoa wa Lindi kwa kushirikiana na serikali ya mkoa huo imegawa sukari ya magendo mifuko elfu tano 319 yenye thamani ya zaidi ya shilingi milioni miatatu kwa taasisi 31 za serikali baada ya kuthibitishwa na Mamlaka ya Chakula na Dawa iko salama kwa matumizi ya binadamu.
Sukari hiyo ilikamatwa mwezi wa pili mwaka huu katika bandari ya Lindi ikiingizwa nchini kinyume cha sheria kutoka Brazil kupitia bandari ya zanzibar.
 
Akizungumza wakati wa ugawaji wa sukari hiyo kwa taasisi za serikali mkoa wa Lindi Mkurugenzi wa huduma na elimu kwa mlipa kodi TRA- Richard Kayombo amesema wamelazimika kuchukua hatua kulingana na sheria inavyowataka.
 
Amesema makubaliano hayo yalifikiwa baina ya TRA na serikali ya mkoa baada ya wenye mali kushindwa kulipa faina na kukomboa mzigo huo ambao mbali na sukari pia meli hiyo ilibeba mafuta ya kupikia,baiskeli,biskuti amira na bidhaa nyingine.
 
Kwa upande wake mwakilishi wa Mkuu wa Mkoa Lindi Hayaya Nawanda ambaye ni Mkuu wa Wilaya ya Lindi amesema serikali ya mkoa huo imejipanga vizuri kiulinzi na kuwaasa wafanyabiashara wa mkoa huo kufanya biashara kwa kufuata sheria za nchi vyinginevyo wataishia pabaya.
 
Download Video and Put Comment
Toa Maoni Hapa Chini

google+

linkedin