Maamuzi hayo yamefikiwa katika mkutano mkuu wa chama hicho ambapo
akizungumza baada ya ufunguzi aliyekuwa mlezi wa chama cha ADC ambaye
pia ni Waziri wa Kilimo Zanzibar,Mhe.Hamad Rashid amesema katiba ya
chama inasisitiza ushiriki katika kugombea nafasi mbalimbali za
uongozi,hivyo kutoshiriki ni kukivunja nguvu chama katika mikakati yake
ya kuchukua dola.
Akizungumza na wajumbe wa mkutano mkuu wa -ADC- Msajili Msaidizi wa
vyama vya siasa Bwana Sisty Nyahoza amesema kitendo cha chama cha siasa
kutoshiriki uchaguzi kinakwenda kinyume na sheria ya vyama vya siasa na
malengo ya kuanzishwa chama Chopchite cha siasa na kusisitiza hipo haja
ya kuangalia mfumo wa usajili wa vyama utakaowezesha kutoa adhabu kwa
vikavyoonekana kukataa kushiriki katika chaguzi.
Aidha mkutano mkuu huo wajumbe wamemchangua aliyekuwa mlezi wa ADC
ambaye kwa sasa ni Waziri wa Kilimo Zanzibar Mhe.Hamad Rashid kuwa
mwenyekiti wa chama hicho taifa na aliyekuwa Naibu Katibu Mkuu wa chama
hicho Bwana Doyo Hassan Doyo amechaguliwa kushika wadhifa wa katibu mkuu
wa chama.
Download Video and Put Comment
Toa Maoni Hapa Chini