Wabunge
wameendelea kuijadili bajeti ya wizara ya ujenzi,uchukuzi na
Mawasiliano huku kiongozi mkuu wa kambi ya upinzani Bungeni Mhe.Freeman
Mbowe akiliambia bunge hilo kuwa msimamo wa kambi hiyo ni kumtaja
hadharani na kumshutumu mtu yeyote ambaye alishiriki ama anashiriki
katika kulihujumu taifa bila kujali kama yupo Serikalini ama kambi ya
upinzani.
Kiongozi huyo mkuu wa kambi hiyo ya upinzani amesema hayo kufuatia
wabunge kupitia chama cha mapinduzi kumshutumu aliyekuwa Waziri mkuu
wakati uuzaji wa nyumba hizo za Serikali Mhe.Edward Lowasa ambaye sasa
ni mjumbe wa kamati kuu ya chadema kuwa naye alishiriki katika uuzaji wa
nyumba hizo kwani Rais wa sasa Dr.John Magufuli alikuwa waziri wa
ujenzi na Mhe.Lowasa alikuwa bosi wa Dr.Magufuli kama Waziri Mkuu.
Download Video and Put Comment
Toa Maoni Hapa Chini