.
Serikali
ya wilaya ya Kilwa mkoani Lindi imemuagiza mkuu wa upelelezi wa wilaya
hiyo kuchukua maelezo ya kina , ikiwa ni pamoja na kuwahoji maafisa wa
TRA bandari na walinzi wa bandari ya Kilwa baada ya Luninga 288 aina ya
flat screen kukutwa zikiwa zimefichwa katika choo no 3 na namba nne
bandarini.
Luninga hizo zimetokana na shehena ya mzigo wa mfanyabiashara
aliyefahamika kwa jina la Teachea kukamatwa katika Bandari ya Kilwa
ukitokea zanziba baada ya kutiliwa mashaka haujalipiwa kodi na hivyo
kuhifadhiwa katika ghala la bandari hiyo.
Akizungumza mara baada ya kuvamia ghafla bandarini baada ya kupata
taarifa za kuwapo mzigo huo Mkuu wa Wilaya ya Kilwa Juma Njuwayo
anasema ripoti za kiiteljensia zinaonyesha kuna wizi katika bandari
hiyo unaofanywa na maafisa wa bandari hiyo.
hata hivyo Meneja wa TRA wilayani Kilwa Titus Shindano ameonyesha
kushangazwa na hilo na kusema mara zote amekuwa akionyeshwa mzigo
uliyopo ghalani na si vinginevyo.
Download Video and Put Comment
Toa Maoni Hapa Chini