Mara yaweka mkakati madhubuti kuwalinda wajawazito | nyula blog

Habari Kila Pande

Breaking News
Loading...

Wednesday, May 18, 2016

Mara yaweka mkakati madhubuti kuwalinda wajawazito


Mkuu wa Mkoa wa Mara Bw. Magesa Mulongo.
Mkakati huo wa mkoa wa Mara unalenga kupambana na vifo vya wanawake wajawazito na watoto chini ya miaka mitano.
Agizo hilo limetolewa wilayani Bunda na Mkuu wa mkoa wa Mara Bw. Magesa Mulongo, kwa nyakati tofauti wakati akizungumza na wananchi wa vijiji vya kata za Kabasa, Wariko na Nyansura wilayani humo Mkoani Mara ikiwa ni sehemu ya ziara yake ya kujitambulisha katika mkoa huo
Amesema licha ya vituo vya Afya na Zahanati kuwa mbali na makazi ya watu katika baadhi ya maeneo lakini endapo viongozi hao wa vitongoji na mitaa watawatambua wajawazito walipo katika maeneo yao wana uwezo mkubwa wa kuweka mipango maalum ya kuwaondolea matatizo hayo wanawake wajawazito hasa wakati wa kujifungua.
Kuhusu tatizo la njaa na upungufu wa chakula mkoani Mara, mkuu huyo wa mkoa wa Mara amewagiza viongozi kuwakamata watu wote wanashindwa kujishughulisha na kilimo huku akisema mkoa wa Mara kwa sasa hauwezi tena kuomba chakula kutoka Serikalini.
Katika hatua Nyingine imegiza kukamatwa na kufunguliwa kesi za ubakaji wanaume ambao watabainika kuwashawishi na kuwapa mimba wanafunzi ikiwa ni pamoja na kuwakamata na kuwafungulia mashitaka wazazi ambao wamekuwa wakijihusisha kuwaficha wanaume wa aina hiyo.
Kiongozi huyo wa mkoa wa Mara amewaonya viongozi wa vijiji, kata na polisi ambao wamekuwa wakitumia ofisi za umma kusuluhisha kesi zinazohusiana na mimba za wanafunzi badala ya kuwakamata watuhumiwa na kuwafikisha mahakamani ili waweze kupata adhabu kali.
Download Video and Put Comment
Toa Maoni Hapa Chini

google+

linkedin