Tanzania
inatarajiwa kusajili kiwango cha juu zaidi cha ukuaji wa uchumi wake
mwaka huu katika kanda ya Afrika Mashariki na kati. Hii ni kwa mujibu wa
ripoti ya shirika la fedha la kimataifa - IMF.
Katika
ripoti yake iliyotolewa jana Tanzania inatarajiwa kusajili kiwango cha
juu cha ukuaji wa uchumi wake wa asilimia 6.9% mwaka 2016.
Kasi
hiyo ya ukuaji wa uchumi wa Tanzania ni ya pili tu nyuma ya Ivory Coast
baina ya mataifa ya Kusini mwa jangwa la Sahara .Ivory Coast
inatarajiwa kukuwa kwa kasi ya asilimia 8.5%.
Katika kanda ya Afrika Mashariki ,uchumi wa Kenya ndio wa pili kwa kasi ya ukuaji kwa asilimia 6%.
IMF
hata hivyo inasema kuwa kasi ya ukuaji wa uchumi kusini mwa jangwa la
Sahara unatarajiwa kupungua kwa mwaka wa pili mfululizo kutokana na
kudorora kwa viwango vya uzalishaji na hivyo uwekezaji.
Kwa
mujibu wa shirika la fedha la kimataifa - IMF, eneo hilo linakadiria
kushuka kwa ukuwaji wa uchumi kwa asilimia 3 mwaka huu.Kiwango hicho ni
cha chini kabisa kuwahi kushuhudiwa katika miaka 15.
Mataifa
yanayotegemea mapato yanayotokana na mafuta ndiyo yalioathirika zaidi
kama vile Nigeria na Angola. Aidha Zambia pia imeathirika vibaya
kutokana na ukosefu wa soko la kimataifa la shaba yake.
Ripoti hiyo inaitaja Afrika Kusini kama moja ya mataifa ambayo kiwango chake cha ukuaji kimedorora kwa kiasi kikubwa mno.
Katika
orodha ya mataifa yanayotarajiwa kuwa na kiwango cha juu cha ukuaji
Kusini mwa jangwa la sahara Ivory Coast ndio inayoongoza.
Orodha ya mataifa ya kanda ya Kusini mwa Jangwa la Sahara na viwango vya kasi ya ukuaji wa uchumi 2016.
- Ivory Coast 8.5%
- Tanzania 6.9%
- Senegal 6.6%
- Kenya 6%
- Zambia 3.4%
- Nigeria 2.3%
- Afrika Kusini 0.6%
Credit: BBC
Download Video and Put Comment
Toa Maoni Hapa Chini