Bodi ya Filamu Tanzania imesitisha usambazaji wa filamu ya “Imebuma” mpaka pale maudhui yake yatakapofanyiwa marekebisho.
Akisitisha
usambazaji wa filamu hiyo, Katibu Mtendaji wa Bodi ya Filamu Tanzania
Bi Joyce Fisso amesema mtengenezaji wa filamu hiyo hana kibali cha
kutengenza filamu kutoka Bodi ya Filamu na hajazingatia Sheria na kanuni
za utengenezaji wa filamu.
Bi
Joyce Fisso amesema filamu hiyo imesitishwa kwenda sokoni kutokana na
kukiuka vifungu vya kanuni za sheria ya Filamu na Michezo ya Kuigiza ya
mwaka 2011 ambayo inakataza kuonesha namna yoyote ya udhalilishaji wa
kibinadamu katika filamu na maigizo.
“Baada
ya kuangalia kwa makini filamu hii na kuona mapungufu ambayo
yanakinzana na Kanuni za Sheria ya filamu na Michezo ya kuigiza
nimeamua kuisitisha usambazaji wake mpaka pale wahusika
watakaporekebisha maudhi yake” Alisema Bi Joyce.
Bi
Joyce amefafanua kuwa filamu hiyo imeonesha baadhi ya matukio ya
udhalilishaji wa kibinadamu, ushawishi wa matendo ya ngono na ushoga
ambayo ni kinyume na madili ya mtanzania.
Aidha
kwa upande wake Afisa Utamaduni kutoka Bodi ya Filamu Tanzania Bw.
Julius Tairo amewataka waandaaji na waigizaji wa filamu nchini kufanya
utafiti wa kutosha kuhusu maudhui ya filamu kabla ya kutengeneza ili
kuondokana na utengenezaji wa filamu zisizofata Sheria na kanuni za
utengenezaji wa filamu Tanzania.
Muhusika
Mkuu katika filamu ya “Imebuma” Bw. Eliasa Mkaly (Rashidi kisoda)
akimbembeleza muigizaji na mtayarishaji wa filamu hiyo Bi Sarah Nyika
(Asha Mauno) mara baada ya Bodi ya Filamu Tanzania kusitizasha
usambazaji wa filamu hiyo leo. Picha na Raymond Mushumbusi MAELEZO
Download Video and Put Comment
Toa Maoni Hapa Chini