Jeshi
la Polisi limetanda mitaa yote ya Kariakoo jijini Dar es Salaam kwa
lengo la kuwadhibiti wafanyabiashara ndogondogo maarufu kama wamachinga
wasipange bidhaa zao chini hatua ambayo wamachinga hao wameipinga kwa
kuanza kurusha mawe ovyo na kusababisha baadhi ya wamiliki wa maduka
kufunga maduka yao na ili kuepousha uwezkekano wa kutokea mdhara zaidi.
ITV ilifika mitaa ya kariakoo na kusuhudia gari za polisi zikipita
huku na kule na baadhi ya wamachinga hao wakizomea na kupiga miluzi
ovyoovyo hataua ambayo ilikuwa kama ni ishara ya kuwachokoza polisi
ambao kila mara walilazimika kufuata makundi mbalimbali ya watu na
kuwatawanya.
Baadhi ya wafanyabishara hao wamesema siyo kwamba wanapinga
kuondoka kariakoo bali ni namna ambavyo wanaondolewa kama vile wao ni
takataka.
Hata hivyo baadhi ya wafanyabiashara hao wamepongeza kitendo cha
kuondolewa katia mitaa hiyo kwani kwa sasa mandhari yamebadilika na hata
magari pamoja na watu wanapita katika njia zao kwa urahisi zaidi.
Kwa upande wake mwenyekiti wa jumuiya ya wafanyabiashara nchini Bw
Filimini Romano amelani Kitendo cha baadhi ya wamachinga kurusha mawe
na kusababisha baadhi ya maduka kufungwa na kusema kitendo hicho siyo
cha kiungwana.
Download Video and Put Comment
Toa Maoni Hapa Chini