Mwalimu
wa Shule ya Msingi Nyaigabo iliyopo Kijiji cha Musati wilayani
Serengeti, Mkoa wa Mara anatuhumiwa kumkuwadia kijana anayemuuzia duka
kwa
kumpelekea mwanafunzi na kusababisha apate ujauzito.
Kamanda wa Polisi Mkoa wa Mara, Ramadhani Ng’hazi alisema mwalimu huyo, Agness Matiko amekamatwa na kuhojiwa kwa tuhuma hizo.
Ng’hanzi
alisema binti huyo mwenye umri wa miaka 16 alimaliza darasa la saba
mwaka jana kwenye shule anayofundisha mwalimu huyo.
Alisema
mwalimu huyo alikuwa akimtoa darasani mwanafunzi na kumpeleka nyumbani
kwake na kumkutanisha na kijana wake huyo kwa ajili ya kufanya naye
ngono.
Binti huyo alikuwa anasoma kidato cha kwanza katika Shule
ya Sekondari Ikorongo kabla ya kufukuzwa baada ya kubainika kuwa na
mimba ya miezi sita.
“Mwaka jana nikiwa darasa la saba mwalimu
alinipeleka nyumbani kwake ili nikamsaidie kukamua ng’ombe maziwa, siku
ya pili wakati wa mapumziko alinichukua nikamuoshee vyombo tulimkuta
huyo kijana baadaye mwalimu alinisihi nibaki naye ndani,” alidai.
Alidai
licha ya kukataa kufanya naye ngono, lakini mwalimu alimwambia: “Mimi
ni mwalimu wako, kama lingekuwa jambo baya nisingekushauri, hivyo wewe
kubali, akatufungia kwa nje. Huyo kijana akanipeleka chumbani kwake
akanilaza kitandani na kuniingilia.”
Kwa mujibu wa mwanafunzi
huyo baadaye mwalimu huyo alikwenda kufungua mlango na kumchukua na
kumpeleka darasani na huo ukawa mwendelezo wa kumkutanisha na kijana
huyo.
Alidai kila mara alimpeleka nyumbani kwake na kuwakutanisha huku akimwambia anataka waoane.
“Baada ya kubainika nina ujauzito walimtorosha huyo kijana na kudai kuwa walimfukuza kwa madai aliwatia hasara dukani,” alidai.
Akizungumza
baada ya kupata dhamana, licha ya kukiri kukamatwa kwa tuhuma hizo,
mwalimu Matiko alisema hajawahi kumfanyia ukuwadi mwanafunzi huyo.
Alisema
kijana aliyekuwa akiishi kwake walimpata kijijini hapa akiwa anatafuta
kazi. “Ndipo tulimpatia kazi ya kuuza duka tangu Aprili hadi Oktoba 2015
nilipomfukuza kwa kunisababishia hasara na alisema kwao ni Mabatini
mkoani Mwanza,” alisema.
Baba wa binti huyo, Marwa Nchama (53)
alisema baada ya kubaini ana mimba alifuatilia na kubaini mwanaye
alikuwa akifanyiwa vitendo vya unyanyasaji na kijana huyo.
Mwalimu
Mkuu wa shule hiyo, Turuka Samwel alikana kulifahamu tukio hilo
likiwamo suala la walimu kuwafanyisha kazi wanafunzi majumbani mwao.
Mkuu
wa Wilaya hiyo, Maftah Ally, alisema watumishi wanaohusishwa na tuhuma
za kuwapa mimba wanafunzi licha ya kufikishwa mahakamani, watawachukulia
hatua za kinidhamu.
Download Video and Put Comment
Toa Maoni Hapa Chini