SERIKALI
ya China imeiunga mkono serikali katika mkakati wake wa kutoa elimu
bure, ikisisitiza kuwa chini ya uongozi wa Rais John Magufuli, Tanzania
inasifika duniani.
Katika kuunga mkono elimu bure, ubalozi wa nchi hiyo nchini umetoa msaada wa madawati 400 yenye thamani ya zaidi ya Sh milioni 28 kwa shule mbalimbali za msingi katika wilaya ya Iramba mkoani Singida.
Balozi
wa China hapa nchini, Dk Lu Youq’ng alisema msaada huo ni moja ya
juhudi za nchi yake kuiunga mkono Serikali ya Tanzania katika kutoa
elimu bure.
“Wakati mimi nimechangia madawati 300, Kampuni inayochimba madini hapa ya Sun Shine Group imechangia madawati 100 ili kuniunga mkono,” alifafanua.
“Wakati mimi nimechangia madawati 300, Kampuni inayochimba madini hapa ya Sun Shine Group imechangia madawati 100 ili kuniunga mkono,” alifafanua.
Akikabidhi
madawati hayo katika mikutano mitatu tofauti kwenye mji wa Kiomboi,
Shelui na Misigiri, Balozi Youq’ng alisisitiza umuhimu wa Tanzania
kuwekeza kwenye elimu kuwaletea wananchi wake maendeleo ya kweli.
“Hata
kama nchi ni maskini kiasi gani, lazima elimu itiliwe mkazo; tena iwe
ni elimu bora na elimu bora haiwezi kuja kwa wanafunzi kukaa chini.
“Madawati ni moja ya mambo ambayo yanamjengea mwanafunzi mazingira
mazuri ya kujifunzia,” alisema.
Aliongeza,
“kutokana na umuhimu huo, ndio maana mbunge wenu aliponijia na kuniomba
msaada wa madawati, sikusita hata kidogo. Nilijua anafanya hivyo ili
kuisaidia jamii yake kuboresha elimu”. Aliyeomba msaada huo ni Mbunge wa Iramba Magharibi, Mwigulu Nchemba.
Aidha,
balozi huyo amewapongeza wakazi wa mkoa wa Singida kwa kumchagua Dk
Magufuli kuwa Rais na kuongeza kusema kuwa chini ya uongozi wake sasa
Tanzania inasifika duniani kote. “Nitahakikisha nchi yangu inaendelea kusaidia maendeleo ya nchi hii kwa kuwa urafiki wetu ni wa enzi na enzi,” alisema.
Download Video and Put Comment
Toa Maoni Hapa Chini