Diwani wa Mtibwa wilayani Mvomero, Lucas Edward (38) maarufu Mwakambaya
anashikiliwa na Polisi Mkoa wa Morogoro kwa tuhuma za kumbaka binti wa
miaka 14, mkazi wa Turiani kwenye nyumba ya kulala wageni.
Kamanda
wa Polisi mkoani Morogoro, Ulrich Matei alisema kuwa mtuhumiwa huyo
alikamatwa Mei 29 saa 12 jioni kwenye nyumba hiyo iliyopo Mtaa wa
Sultan, Manispaa ya Morogoro.
Matei alisema polisi walipata
taarifa kutoka kwa msiri wao kwamba katika nyumba hiyo, kuna mtu
ameonekana akiwa na binti mdogo, hivyo askari walifuatilia nyendo zake
na kumkamata.
Alisema askari baada ya kufika kwenye nyumba hiyo, walimkuta mtuhumiwa huyo akiwa na binti huyo chumba namba 108.
Alisema uchunguzi wa kitabibu unaendelea kuthibitisha tuhuma hizo.
Akizungumza
kwa simu, Katibu wa Chama cha Demokrasia na Maendeleo (Chadema) Wilaya
ya Mvomero, Mrisho Ramadhan alithibitisha kukamatwa kwa diwani huyo na
kwamba mpaka sasa hajafahamu ni kwa tuhuma gani.
Ramadhan
alisema kwa sasa wao kama viongozi wa chama wanafuatilia kujua tuhuma na
ameomba uongozi wa Chadema Mkoa kufuatilia zaidi na kwamba, atatoa
taarifa baada ya kufahamu kwa undani.
“Ni kweli nimesikia
mheshimiwa kakamatwa huko mjini Morogoro, sijajua kosa nimewaomba
viongozi wa Mkoa Chadema kufuatilia nitatoa maelezo baadaye,” alisema
Ramadhan.
Alisema baada ya kupata undani wa tukio hilo, atatoa taarifa ili kujulisha umma kilichotokea.
Download Video and Put Comment
Toa Maoni Hapa Chini