Jaribio la kutaka kuuza nyumba ya mama huyo Bi Khadija Issa
lilifanyika mwishoni mwa mwezi April mwaka huu katika eneo la Kaloleni
jijini Arusha baada ya kundi la watu wakiwa na askari wa kampuni binafsi
za ulinzi walivamia nyumba yake na kumtoa nje na kufunga nyumba hiyo.
Pamoja na jaribio hilo kushindwa baadhi ya ndugu na majirani wa
mjane huyo wameiomba serikali kuendelea kuwachukulia hatua baadhi ya
watu wanaoendesha kampeni za kudhulumu mali za wajane na wagane.
Mlezi wa mjane huyo Bw Isumail Issa amelalamikia uharibifu na wizi
wa mali zenye thamani ya dola elfu 30 uliofanyika wakati wa jaribio la
kupora nyumba ya mjane huyo.
Mama huyo mjane aliyetolewa ndani ya nyumba yake hiyo kabla ya
kurejea kwa muda wote amekuwa akiishi kwa majirani akitegemea misaada
ya wasamaria wema.
Download Video and Put Comment
Toa Maoni Hapa Chini