Uhaba
mkubwa wa Sukari katika manispaa ya Musoma umesababisha wananchi
kutumia zaidi ya saa kumi katika foleni za kununua bidhaa hiyo huku bei
yake ikizidi kupanda kutoka shilingi elfu mbili hadi shilingi elfu tano
kwa kilo moja ya Sukari.
Baadhi ya wafanyabiashara wa maduka ya rejareja wa mjini Musoma,
wakizungumza huku wakiwa katika foleni hiyo katika moja ya duka lilokuwa
likiuza bidhaa hiyo katika barabara ya sokoni mjini Musoma, wamesema
wanalazimika kujipanga kwa zaidi ya saa kumi wakisubili kuuziwa mfuko
mmoja wa Sukari wa kilo 50 kutoka nchini Brazil kwa shilingi 130,000.
Hata uchunguzi ambao umefanywa na ITV umebaini kuwa baadhi ya
wafanyabiashara wakubwa wamekuwa wakitoa masharti na kuuza mfuko mmoja
wa Sukari kwa shilingi 130,000 huku wakitoa stakabadhi za shilingi
105,000 kwa wauzaji hao wa rejareja.
Download Video and Put Comment
Toa Maoni Hapa Chini