Watanzania
wamesisitizwa kuwa jukumu la uhakiki wa simu muhimu kwa kila
mmoja,hivyo hawana budi kuhakikisha kuwa simu imehakikiwa kwa pindi hiki
cha mpito kinachomalizika Juni 16 mwaka huu,ili kuzuia usumbufu wa
aina yoyote unaowezakujitokeza wakati kutekeleza azima hiyo.
Rai hiyo imetolewa kwenye taarifa ya Kaimu mkurugenzi mkuu wa
Mamlaka ya Mawasiliano Tanzania(TCRA)Mhandis James Kilaba iliyosomwa kwa
niaba yake na Meneja Mawasiliao(TCRA)Innocent Mungy,wakati wa semina
kwa wadau mbalimbali wa mawasiliano wakiwemo Wauzaji wa Simu na mafundi
simu,iliyofanyika hivi lao mjini Bukoba kwa kushirikisha shirika la
viwango nchini(TBS)pamoja na Tume ya Ushindani(FCC).
Mhandisi Kilaba ameleza kuwa TCRA inaendelea na mpango wa kutoa
elimu kwa umma ili wateja(watumiaji)wa simu kuweza kuhakiki simu
walizonazo au wakati wanataka kununua simu mpya,programu hiyo ya kutoa
elimu kwa umma kutambua simu bandia ilianza kutolewa nchini tangu mwezi
Novemba 2011.
Aidha,amesema kuwa Mamlaka ya Mawasiliano imeendelea pia na
kampeini za kutoa elimu kwa umma kuhusu jinsi ya kuhakiki namba
tambulishi(IMEI)za vifaa vya mkononi(mobile devices),ambapo katika
kampeini hiyo wananchi wameweza kutambua uhalisia wa simu zao ikiwa ni
pamoja na mambo muhimu ya kuzingatia wakati wa ununuzi wa simu.
Aidha,pamoja na mkakati huo unaoendelea kutekelezwa,bado kumetokea
changamoto mbalimbali zikiwemo uamini mdogo kwa baadhi ya
wafanyabiashara wa simu kwa kutoa punguzo kwa wananchi ili kuwashawishi
kuzinunua simu bandia kwa bei nafuu,jambo ambalo limesababisha
kuongezeka simu bandia katika soko kabla ya uzimaji wa simu hizo.
Pia,uelewa mdogo wa baadhi ya wananchi katika kuitikia wito wa
kuhakiki simu zao katika kipindi cha mpito,wananchi wameshindwa kuelewa
umuhimu wa kuhakiki simu zao kabla ya kununua,ni kitu ambacho kinaweza
kusababisha kuongezeka simu bandia katika soko kabla ya uzimaji wa simu
hizo.
Wakati huo huo,Mmlaka ya mawasiliano nchini(TCRA)imeendelea kutoa
onyo kwa wafanyabiashara wa vifaa vya mawasiliano vya mkononi,kuacha
kushawishika kujiingiza katika vitendo vya kubadilisha namba tambulishi
za vifaa vya mkononi,vinginevyo mamlaka haitasita kuwachukulia hatua za
kisheria ambavyo adhabu yake ni faini isiyopungua milioni 30.
Semina hiyo iliywahusisha wafanyabiashara kutoka wilaya za
Bukoba,Muleba,Karagwe na Missenyi pia,wadau wengine wa TBS,FCC pamoja na
jeshi la Polis waliweza kutoa mada mbalimbali juu ya mfumo wa rajis ya
namba za utambulisho wa simu.
Download Video and Put Comment
Toa Maoni Hapa Chini