Mungi ameyasema hayo alipokuwa akiongea na wauzaji na watumiaji wa
simu mkoani Geita amesema hakuna mtu yeyote atakayelipwa fidia pindi
simu zitakapozima hivyo kuwataka wauzaji kuachana na uagizaji na
usambazaji wa bidhaa zisizokuwa na ubora ili kuepukana na madhara
mbalimbali yanayoweza kujitokeza.
Naye mkuu wa mkoa wa Geita Meja Jenerali Ezekiel Kyunga ameyataka
makampuni ya simu kuhakikisha wanaboresha mawasiliano hasa vijijini
kutokana na mahitaji ya muhimu waliyonayo kutokana na changamoto ya
miundombinu.
Baadhi ya wafanyabiashara wa simu mkoani Geita wamesema kwa sasa
biashara yao imeharibika kutokana na taarifa za kuzimwa na kufungiwa kwa
simu bandia na kuomba uongezwe muda kwani mpaka sasa wana mzigo mkubwa
ambao bado ambao haujauzwa.
Download Video and Put Comment
Toa Maoni Hapa Chini