Mwenyekiti
Mtendaji wa IPP Dr. Reginald Mengi ameyasema hayo jijini Dar es salaam
wakati alipokuwa akitoa Mhadhara katika Chuo cha Ulinzi Cha Taifa
Kunduchi jijini Dar es salaam, kuhusu Wajibu wa Vyombo vya Habari
binafsi katika ulinzi wa Taifa.
Amesema viongozi wa serikali kwa kupitia vyombo vyake vinahitajika
kuweka utaratibu wa kukutana mara kwa mara na waandishi wa habari
waandamizi ili kuwafafanulia mambo mbalimbali yanayohusu mustakabali wa
taifa ili kuvipa uwezo vyombo vya habari kutekeleza uzalendo wao kwa
nchi zao kupitia habari wanazoziandika na kutangaza.
Akijibu swali kuhusu uwezekana wa nchi kutekwa nyara na kundi la
watu wachache wenye maslahi binafsi, hususan wakati wa uchaguzi mkuu,
Dr. Mengi amesema jambo hilo linatokea penye rushwa iliyokithiri, na
kusisitiza kuwa dawa yake ni kuzidisha mapambano dhidi ya rushwa.
Mkuu wa Chuo cha Ulinzi cha Taifa Meja Jenerali Yacoub Mohamed
amesema chuo hicho kilichoanzishwa mwaka 2012 hutoa mafunzo ya muda
mrefu na mfupi kwa viongozi waandamizi wa umma na sekta binafsi kutoka
nchini na nje ya nchi:..
Mkuu huyo wa Chuo amesema sasa hivi chuo kinaendesha awamu ya nne
ya mafunzo kwa kuwashirikisha wanachuo 38, wakiwemo Watanzania 26 na
wengine 12 wanatoka nchi za Burundi, Uganda, Kenya, Zambia, Afrika
Kusini, Botswana, Namibia, Nigeria, Malawi na China, lengo likiwa kutoa
mafunzo kwa viongozi waandamizi wa serikali na sekta binafsi.
Download Video and Put Comment
Toa Maoni Hapa Chini