Dkt. Magufuli: Ujenzi wa bomba la mafuta kuanza. | nyula blog

Habari Kila Pande

Breaking News
Loading...

Friday, May 13, 2016

Dkt. Magufuli: Ujenzi wa bomba la mafuta kuanza.



Rais wa Uganda,Yoweri Museveni akisalmia na Rais wa Tanzania Dkt. John Magufuli katika sherehe za kuapishwa kuwa raisa wa Uganda hapo jana nchini Humo.
Rais Dkt. Magufuli pamoja na Rais Museveni wamezungumzia kuharakishwa kwa ujenzi wa Bomba la Mafuta kuanza mara moja kujengwa kuanzia mkoani Tanga mpaka nchini Uganda ili kuanza kazi baada ya miaka miwili ijayo .
Mazungumzo hayo ilikuwa mara baada ya Rais Museveni kuapishwa ambapo awali, akiongea na maelfu ya watu waliohudhuria sherehe za kuapishwa kwa muhula wa tano, rais Museveni, amesema katika kuonyesha haijali Mahakama ya ICC aliamua kumualikia rais wa Sudan Omar Al-Bashir licha ya kuwepo kwa hati ya ICC ya kutaka akamatwe.
Sherehe hizo za kuapishwa rais Museveni, zimehudhuriwa na marais Jacob Zuma wa Afrika Kusini, Robert Mugabe wa Zimbabwe, Idriss Deby wa Chad, Edgar Lungu wa Zambia, John Magufuli wa Tanzania, Mohamadou Issoufou wa Niger na Teodoro Obiang Nguema Mbasogo wa Equatorial Guinea.
Download Video and Put Comment
Toa Maoni Hapa Chini

google+

linkedin