Makamu
wa Rais wa Jamuhuri ya Muungano wa Tanzania Mama Samia Suluhu amewataka
viongozi wa siasa na serikali kufuata taratibu za uwajibishwaji wa
watumishi pindi inapotokea kasoro katika utendaji wao.
Akizungumza na Wauguzi na wananchi wa mkoa wa Geita katika siku ya
wauguzi duniania ambapo kitaifa imefanyika katika mkoa wa Geita Mama
Samia amesema serikali itaendelea kuboresha stahiki na mazingira ya kazi
kila itakapoweza ili kuwafanya watumishi wa umma kufanya kazi katika
mazingira bora.
Naye Waziri wa Tawala za mikoa na serikali za mitaa Mheshimiwa
George Simbachawene amesema atasimamia na kuhakikisha haki za wauguzi
zinapatikana kwa wakati ili kuboresha huduma ya afya nchini.
Awali akisoma risala mbele ya mgeni rasmi Rais wa chama cha wauguzi
Tanzania Paul Magesa amesema mpaka sasa kuna uhaba wa wauguzi kwa
asilimia hamsini na moja tu jambo hili huwafanya wauguzi kufanyakazi
nyingi katika mazingira magumu hivyo kuomba ajira ziongezwe katika sekta
hiyo.
Download Video and Put Comment
Toa Maoni Hapa Chini