Wakichangia bajeti ya wizara ya viwanda, biashara na uwekezaji,
wabunge hao wamesema ipo haja ya mapungufu yaliyopo katika sekta ya
viwanda na biashara nchini yakafanyiwa kazi kwani yanafahamika ila
utatuzi wake umekuwa wa kusuasua.
Baadhi ya wabunge kutoka vyama vya upinzani wamesema serikali
inatakiwa kuweka kipaumbele katika kufufua viwanda vilivyokufa kama
ilivyoahidi kwani watanzania bado wanaimani kuwa vikifufuliwa vitaweza
kufanya vyema.
Naye waziri wa wizara hiyo Charles Mwijage amesema kila
anachokisema bungeni atakitekeleza kwani yeye ni mtu wa vitendo na siyo
maneno na kama kuna mbunge aamini hilo amtafute na aeleze anataka
mwekezaji wa sekta gani na atampata baada ya muda mfupi huku akitoa
baadhi ya maagizo kwa watendaji wa chini wa wizara yake.
Awali bungeni hapo mwenyekiti wa umoja wa wabunge wanawake Magreth
Sitta aliwasilisha maelezo binafsi ya umoja huo na kulaani kauli ya
udhalilishaji waliyoambiwa wanawake wa vyama vya upinzani viti maalum
kuwa wabunge mpaka wawe na uhusiano wa kimapenzi na viongozi wa vyama
vyao.
Download Video and Put Comment
Toa Maoni Hapa Chini