Mtu 1 ameuawa kwa risasi na kusababisha vurugu kati ya polisi na wananchi mkoani Mara. | nyula blog

Habari Kila Pande

Breaking News
Loading...

Monday, May 9, 2016

Mtu 1 ameuawa kwa risasi na kusababisha vurugu kati ya polisi na wananchi mkoani Mara.


Watu kadhaa wakiwemo wagonjwa waliokuwa wamelazwa katika kituo cha afya cha Nyamongo wilayani Tarime mkoani Mara    wamejeruhiwa vibaya kwa kupigwa risasi za moto wakati askari wa jeshi la polisi wakipambana na baadhi ya wakazi wa mji huo walikuwa wakiwazuia polisi kuchukua mwili wa kijana mmoja anadaiwa kuuawa kwa kupigwa risasi na askari wa jeshi la polisi.
Tukio hilo ambalo limesababisha wagonjwa watatu ambao wamelazwa katika kituo hicho cha afya maarufu kama hospitali ya Sungusungu kujeruhiwa vibaya kwa kipigwa risasi, imeelezwa na baadhi ya viongozi wa vijiji katika eneo hilo kuwa askari polisi walianza kurusha risasi baada ya kutofautiana na familia katika kuchukua mwili wa kijana huyo Jackison Mwita. 
 
Kwa upande wake mbunge wa jimbo la Tarime vijijini Mh John Heche ambaye ametembelea mji wa Nyamongo kufuatia tukio hilo, ameonesha kusikitishwa kwa askari polisi hao kuua wananchi kwa risasi kisha   kusababisha vurugu hizo ambazo pia zimesababisha uharibifu mkubwa katika kituo hicho cha afya. 
 
Naye mwenyekiti wa kamati ya ulinzi na usalama Bw Gloriuos Luoga ambaye pia ni mkuu wa wilaya ya Tarime amesema baada serikali kupokea taarifa rasmi ya uchunguzi wa jopo la madaktari, serikali itaunda tume ili kujua kiini cha tukio hilo.
Download Video and Put Comment
Toa Maoni Hapa Chini

google+

linkedin