Mamlaka
ya usafiri wa nchi kavu na majini SUMATRA imetangaza nauli
zitakazotumika katika uendeshaji wa mabasi yaendayo haraka huku
waendesha bodaboda na watumiaji wengine wa vyombo vya usafiri wakipigwa
marufuku kupita katika barabara za mabasi yaendayo haraka jijini Dar es
Salaam.
Umamuzi huo umekuja baada ya majadiliano ya ipi iwe bei ya nauli ya
Mabasi hayo yaendayo haraka, ambapo siku 90 zilitosha kufikiwa kwa
muafaka huku bodi ya SUMATRA ikiamini viwango hivi vya nauli ni rafiki
kwa kila mtanzania.
Mtendaji Mkuu wa DARTS Mhandisi Ronald Lwakatare, amesema kuanzia
sasa hatua kali za kisheria zitaanza kuchukuliwa kwa mtumiaji yeyote wa
chombo cha usafiri atakayepitisha gari, pikipiki, guta,au baiskeli
katika barabara za mabasi yaendayo haraka.
Wakati usafiri mabasi yaendayo haraka ukitarajiwa kuanza muda
wowote kuanzia sasa, baraza la madiwani la jijini la Dar es salaam
lililoketi Mei 2 mwaka huu limepitisha maazimio kadhaa yakiwemo ya
kupinga ununuzi wa hisa zake katika shirika la UDA ambazo ni sawa na
asilimia 51.
Wakazi wa jiji la Dar es Salaam wamepongeza juhudi kubwa za serikali za kuondoa foleni katika jiji hili la Dar es Salaam.
Download Video and Put Comment
Toa Maoni Hapa Chini