Zaidi
ya wafanyakazi 150 wa kampuni ya China Railway Jianchang Engineering
(CRJE), inayojenga miradi mikubwa ya majengo ya vitega uchumi katika
maeneo ya Capripoint na Ghana jijini Mwanza, wamegoma kuingia kazini
wakishinikiza kulipwa malimbikizo ya mapunjo ya mishahara yao ya miaka
mitatu iliyopita pamoja na stahiki zao mbalimbali ikiwemo michango ya
mfuko wa pensheni wa NSSF.
Wafanyakazi wa kampuni hiyo ya CRJE waliogoma kuingia kazini ni
wale wanaojenga jengo la Rock City Shopping and More lililopo eneo la
Ghana, ambalo ni mradi wa mfuko wa pensheni wa LAPF na wenzao
wanaoendelea na mradi wa ujenzi wa hoteli ya kitalii yenye hadhi ya
nyota tano ya ghorofa kumi na sita, ambayo ni kitega uchumi cha mfuko wa
pensheni wa NSSF, mradi huo unatarajia kukamilika mwezi Novemba mwaka
huu.
ITV pia imefika katika mradi wa uwekezaji mkubwa wa jengo la Rock
City Shopping and More mtaa wa Ghana na kuwakuta wafanyakazi zaidi ya 70
wakiwa wameweka chini zana zao za kazi ambapo baadhi ya wafanyakazi hao
walikuwa na haya ya kusema kuhusiana na mgomo huo.
Katibu wa chama cha wafanyakazi wa migodi, nishati na ujenzi
(STAMICO) kanda ya ziwa, Paterinusi Rwechungura amefika katika eneo la
Capripoint na kuzungumza na wafanyakazi hao.
Meneja mradi wa kampuni ya CRJE Li bo, kupitia kwa mkalimani wake
Bwani Bwakeha amesema wamezingatia madai ya wafanyakazi hao na taratibu
za uhakiki wa malipo yao zilipangwa kuanza hii leo mchana kuanzia majira
ya saa nane mchana.
Download Video and Put Comment
Toa Maoni Hapa Chini