Mwenge
wa Uhuru unanarajiwa kuwashwa Kitaifa mkoani Morogoro mapema April18
Mwaka huu ambapo zaidi ya bilioni Miatisa na Milioni Miatatu zimetumika
kwa matumizi ya miradi 41 ambayo itazinduliwa huku mingine ikiwekwa jiwe
la Msingi.
Akizungumza wakati wa kupokea msaada wa sare za nguo za kuvaa
watoto kwenye Mwenge zilizo tolewa na benki ya NMB kanda ya Mashariki
mkuu wa mkoa wa Morogoro Stephan Kebwe amesema maandalizi ya Mwenge yako
vizuri na viongozi mbalimbali wakiwemo wakuu wa wilaya wa mejipanga
kuhudhuria uzinduzi huo.
Kwaupande wake meneja wa NMB kanda ya Mashariki Nazareth Lebby
amesema wametoa mabosi 20 ya nguo za kuvaa vijana katika Mwenge yenye
thamani ya zaidi ya shilingi milioni 34 ikiwa ni mchango wao katika
kufanikisha kuwasha mwenge mkoani Morogoro.
Aidha katika hatua nyingine benki ya NMB tawi la wami mkoani
Morogoro wametoa msaada wa madawati 50 katika shule ya sekondari lupanga
ambapo shule hiyo ilikuwa na uhaba wa madawati 90 na kwa kupata hayo
yatasaidia kupunguza usumbufu wa wanafunzi kukosa pakukaa.
Download Video and Put Comment
Toa Maoni Hapa Chini