Mwenyekiti wa kamati ya ulinzi na usalama wilaya ya Kahama Bw.Vita 
Kawawa,amesema katika tukio hilo raia mwingine mmoja alipigwa risasi na 
majambazi hao na kupoteza maisha wakati akipelekwa hospitali huku 
akilipongeza jeshi la polisi kwa kazi nzuri waliyoifanya.
Akizunguymza kwa njia ya simu  kaimu Kamanda wa Jeshi la Polisi 
mkoani Shinyanga ACP Dismas Kisusi amethibitisha kutokea kwa tukio hilo 
na kuwataka wananchi kutoa ushirikiano wa kutosha kwa jeshi la polisi 
punde wanapoona dalili zozote za kiuhalifu zinafanyika.
Katika tukio hilo jeshi la polisi limefanikiwa kukamata bunduki 
mbili moja aina ya Shotr Gan na moja ya kivita aina ya Uzgun,bomu la 
kutupa kwa mkono, kisu cha kijeshi,risasi sitini,mkandawa kijeshi na 
magazine mbili za bunduki.
 Download Video and Put Comment
 Toa Maoni Hapa Chini