Wanawake
wawilivikongwe wameuawa kinyama kwa kupigwa na kukatwakatwa kwa mapanga
kisha miili yao kuchomwa moto katika kijijicha Kenyamsana wilayani
Rorya mkoani Mara kwa tuhumu za kujihusisha na ushirikina,tukio ambalo
limesababisha hofu kubwa kwa wanawake wengi wenye umri mkubwa katika
kijiji hicho.
Wakizungumzia tukio hilo la kwanza kutokea wilayan Rorya, baadhi ya
ndugu wa marehemu hao, wamesema kuwa kundi la watu waliwakamata
wanawake hao vikongwe kisha kuwapiga katika sehemu mbalimbali za
miili huku wakiwaingiza kwa nguvu ndani ya nyumba zao ambazo zimeezekwa
kwa kutumia nyasi na kuwachoma moto.
Kufutia tukio hilo la kusikitisha na la kikatili Mwenyekitiwa
kamati ya ulinzina usalma ambaye pia ni mkuu wa wilaya ya Rorya Bw Felix
Lyaniva, amefika eneo la tukio na kuliagiza jeshi la polisi kuwakata
watu wote ambao wamehusika kufanya kitendo hicho cha kinyama kwa
kuanzia na viongozi wa vitongoji katika eneo hilo.
Tayari Jeshi la Polisi limewakamata watu 13 kwa tuhuma za kuhusika
na mauaji hayo ya wanawake hao vikongwe Bi Ghati Ndege na Nyakorema
Waryuba wote wakazi wa k ijiji hicho cha Kenyamsana wilayani Rorya.
Download Video and Put Comment
Toa Maoni Hapa Chini