Waziri
mpya wa Ujenzi, Mawasilaino na usafirishaji wa Zanzibar Balozi Ali
Abeid Karume amewatahadharisha wafanyakazi wa wizara hiyo kuweka siasa
pembeni na kuchapa kazi huku akiahidi hatofanya kazi kwa fitna na
majungu na kuangalia itikadi za chama.
Balozi Karume ametoa tahadhari hiyo wakati wa makabidhiano ya
wizara hiyo kutoka kwa waziri wa mwanzo wa awamu iliyopita ambapo
amesema huu si wakati wa kuhoji mfanyakazi anatoka chama gani ndipo
apewe huduma ila ni wakati wa kuwatumikia wananchi na kuwapa huduma
muhimu zote za kijamii zinazotokana na wizara hiyo ambayo inagusa hisia
za watu wa rika zote.
Akizungumzia utendaji wa wizara Balozi Ali Karume amesema yeye ni
mchapakazi ambaye anapenda kuwasikiliza wale anaofanyakazi nao na kuonya
hatovumulia, mambo ya fitna na majungu ila anataka ushirikiano, kwa
upande wake aliyekuwa naibu waziri wa wizara hiyo ya Mawasiliano Issa
Haji ambaye alikabidhi kutokana na wizara hiyo kutokuwa na waziri baada
ya kujiuzulu kwa Mhe Juma Duni amesema ana imani kuwa wizara hiyo mpya
imepata mtaalamu na msomi na mwenye ujuzi wa kuendeleza wizara hyo.
Kikosi hicho kipya cha mawaziri wa Dr Shein mawaziri wake wamekuwa
wakianza kwa kishindo na kutahadharisha kuwa huu si wakati wa siasa tena
ila ni wa kuchapa kazi.

Download Video and Put Comment
Toa Maoni Hapa Chini