Wawekezaji
kutoka nchi ya Oman wameahidi kuwekeza katika mashamba makubwa
yanayotumiwa na serikali kwa ajili ya kuhudumia mifugo yaliyopo katika
maeneo mbalimbali nchini ili kukuza pato la taifa sanjari na kuuza
bidhaa zitokanazo na sekta ya kilimo na ufugaji katika nchi hiyo.
Mratibu wa timu ya wawekezaji waliofika nchini kwa ajili ya
kujifunza na kukagua maeneo ambayo yatawapa fursa ya kuwekeza katika
sekta ya ufugaji na kilimo, Warith Al Khamis amesema hatua hiyo
itaongeza ajira hata kwa watanzania na kutoa mfano kuwa eneo la shamba
walilotembelea lenye hekta 5000 lina Ng'ombe 2500 tu idadi ambayo
haitoshelezi mahitaji ya ardhi iliyopo.
Kwa upande wake mtendaji mkuu wa wakala wa maabara ya Vetenari
nchini iliyo chini ya wizara ya kilimo, mifugo na uvuvi Dr,Furaha Mramba
amesema tayari wamekaa na wawekezaji wa Oman mapema mwaka jana
walikubaliana kuwekeza katika shamba la Mivumoni lililopo wilayani
Pangani kwa kuwekeza katika kilimo cha majani ya chakula cha mifugo na
kuuzwa falme za kiarabu.
Kufuatia hatua meneja wa taasisi ya utafiti wa wadudu na magonjwa
waenezayo kwa mifugo iliyopo chini ya wakala wa maabara za Vetenari
nchini Dr, Imna Malele amesema kuwa endapo zoezi hilo litafanikiwa
wameandaa mpango wa kulisha mifugo kutoka maeneo mbalimbali kulingana na
utaratibu utakaowekwa ili kupunguza wafugaji kuswaga mifugo yao na
kulisha katika mashamba ya wakulima na kusababisha migogo baina ya pande
hizo mbili.
Download Video and Put Comment
Toa Maoni Hapa Chini