Wazazi na walezi wametakiwa kukagua mabegi ya watoto wao
wanapotoka shuleni na wanapokwenda kwa lengo la kuhakikisha usalama wao
na kupata picha halisi ya wanachokifanya shuleni.
Hayo
yamesemwa na Kungwi maarufu katika eneo ka Kinondoni Mosko jijini Dar
es salaam Bi. Chambua alipokuwa akizungumza na Uswazi kipindi
kinachorushwa na kituo cha EATV.
''Wazazi hawafahamu tu, watoto siku hizi wanaweka nguo mbili kwenye mabegi akiondoka asubuhi begi kubwa unadhani anakwenda shuleni kumbe akitoka anabadilisha nguo anaingia kwenye mageto huko akirudi jioni anakuwa kavaa sare za shule kama kawaida''-Amesema Bi Chambua.
Bi. Chambua ameongeza kuwa kuna tofauti ya kunwi na 'kitchen party' kwamba kwenye sherehe hiyo binti hukabidhiwa vyombo tuu lakini hakuna mahusia anayopata ya msingi kama wanayotoa kungwi ya kumwelekeza mwali namna ya kuishi na mumewe na kuheshimu ndugu za mume bila ubaguzi.
Kungwi ni moja ya kazi zinazosifika sana maeneo ya uswahilini ambapo wanawake wengi hupenda mabinti zao wafundwe kabla ya kuolewa ambapo kungwi ndo hupewa kazi hiyo ya kumueleza binti namna ya kuheshimu mume na kumjali na kutambua mambo muhimu yanayoweza kusambaratisha ndoa.

Download Video and Put Comment
Toa Maoni Hapa Chini