Afya
za baadhi ya wakazi wa wilaya ya Handeni zipo hatarini kufuatia baadhi
ya wakazi wake kukaidi kuchimba vyoo na badala yake baadhi yao
wanajisaidia Pembeni mwa Bwawa hilo lenye maji yanayotumika na sehemu
kubwa ya wakazi wa mji wa Chanika wilayani humo kisha vinyesi vyake
huteremshwa na maji ya mvua hadi katika bwawa hilo huku wengine
wakiyatumia bila kuyachemsha.
Akizungumza katika mahojiano maalum na ITV kuhusu mikakati
iliyowekwa na idara ya Afya ya kukabiliana na magonjwa ya milipuko hasa
katika kipindi hiki cha mvua za masika,mganga mkuu wa wilaya ya Handeni
Dr,CrediaNus Mgimba amewataka wakazi wanaolima pembeni mwa bwawa hilo
kuacha kujisaidia katika vichaka ili kudhibiti milipuko ya ugonjwa wa
homa za matumbo na kipindupindu wilaya Handeni.
Baadhi ya wakazi waliokutwa katika Bwawa hilo wakiteka maji ambapo
baadhi yao wanakwenda kuuza kwa wananchi huku wengine ni kwa ajili ya
matumizi ya kila siku,wamesema kuwa wanatambua kuwa maji hayo sio salama
hivyo wameiomba serikali kuboresha miundo mbinu ya bwawa hilo ili
kuzuia mtiririko wa vinyesi vinavyokwenda katika maji ili kunusuru afya
za wanachi.
Kufuatia hatua hiyo,mkuu wa wilaya ya Handeni Husna Msangi
amewataka wananchi kuzingatia kanuni za afya ili kuepuka magonjwa ya
milipuko ikiwa ni pamoja na kuchimba vyoo,kuchemsha maji ya kunywa na
kunawa mikono kwa kutumia sabuni baada ya kujisaidia.
Download Video and Put Comment
Toa Maoni Hapa Chini