SERIKALI
imeanza kulipa deni la mifuko ya hifadhi ya jamii na hadi kufikia
Machi, mwaka huu tayari imeshalipa Sh bilioni 173.11 kwa mfuko wa PSPF
huku ikidhamiria kulipa deni lote kufikia Juni, mwaka huu.
Kwa
mujibu wa taarifa iliyotolewa na Mamlaka ya Usimamizi na Udhibiti wa
Sekta ya Hifadhi ya Jamii (SSRA) mfuko huo pia umeweza kulipa hundi
49,467 na kati ya hizo 46,000 ni za pensheni za kila mwezi kwa wastaafu
na 3,467 za madai mapya.
Aidha,
taarifa hiyo inaeleza kuhusu hati fungani, mifuko ambayo ilikuwa bado
haijaridhia hati ya makubaliano kwa sasa zimesharidhia.
“Serikali
inatarajia kutoa Hati Fungani ya Sh trilioni 2.6 yenye riba ya asilimia
6.5 kwenda PSPF. Hati fungani hizi zitaiva kwa vipindi tofauti, kuna za
miaka mitatu, mitano, saba, 10 na kuendelea,” ilieleza taarifa hiyo.
Kwa
upande wa miradi ya uwekezaji, Mamlaka hiyo kwa kushirikiana na Benki
Kuu (BoT) kwa mujibu wa sheria ilikamilisha ukaguzi wa mifuko kwa mwaka
2015.
Ukaguzi
huo ulisababisha mamlaka kwa kushirikiana na BoT kufanya ukaguzi
maalumu kwenye majengo na milki za mifuko yote ya hifadhi ya jamii
ukiwemo wa NSSF.
Aidha,
ukaguzi huo unatarajiwa kuchukua kati ya miezi hadi tisa kulingana na
upatikanaji wa taarifa na kwamba wakati kaguzi hizo zikiendelea mifuko
iliyovuka viwango vya uwekezaji imezuiwa kuendelea kuwekeza katika
maeneo hayo.
Taarifa
hiyo pia ilieleza kuwa mifuko imeonekana kuwa na gharama kubwa ya
uendeshaji na kwamba kuwepo kwa gharama hizo kutazorotesha utendaji wa
mifuko ya hifadhi ya jamii.
Download Video and Put Comment
Toa Maoni Hapa Chini