Rais
wa Jamhuri ya Muungano wa Tanzania Dkt. John Pombe Magufuli ametengua
uteuzi wa Mhariri Mtendaji wa Magazeti ya Serikali (TSN) Bw. Gabriel
Nderumaki.
Taarifa
iliyotolewa leo tarehe 14 Aprili, 2016 na Katibu Mkuu Kiongozi Balozi
Mhandisi John Kijazi, imeeleza kuwa Rais Magufuli ametengua uteuzi huo
kuanzia tarehe 18 Machi, 2016.
Kufuatia kutenguliwa kwa uteuzi huo, Rais Magufuli amemteua Bi. Tuma Abdallah kukaimu
nafasi hiyo.
Bi. Tuma Abdallah ni Mhariri Mtendaji Msaidizi wa Magazeti ya Serikali (TSN)
Gerson Msigwa
Kaimu Mkurugenzi wa Mawasiliano, IKULU
Dar es salaam-14 Aprili, 2016
Download Video and Put Comment
Toa Maoni Hapa Chini