Waziri
wa Nchi katika Ofisi ya Rais, Tawala za Mikoa na Serikali za Mitaa
(Tamisemi), George Simbachawene amevunja bodi ya Soko la Machinga
Complex lililopo Ilala Mchikini Dar es Salaam na kulikabidhi kwa mkuu wa
mkoa wa Dar es salaam, Paul Makonda.
Akizungumza
leo katika mkutano wa Jumuiya ya Wafanyabiashara nchini (JWT),
Simbachawene amesema wazo la kuanzishwa kwa soko hilo lilikuwa zuri
lakini Halmashauri ya Jiji la Dar es Salaam imeshindwa kulitekeleza.
Jengo
hilo lilikamilika kujengwa mwaka 2010 likiwa na uwezo wa kuchukua
wafanyabiashara 4206, lakini Waziri Simbachawene alisema limeishia kuwa
makazi ya popo
Download Video and Put Comment
Toa Maoni Hapa Chini