Mahakama ya Hakimu Mkazi Kisutu jijini Dar es Salaam leo imewaachia huru aliyekuwa Mkurugenzi Mkuu wa Shirika la Umeme Tanzania (Tanesco), William Mhando na mkewe Eva Mhando .
Mhando
na wenzake walikuwa wanashitakiwa kwa makosa sita likiwemo la matumizi
mabaya ya ofisi, kughushi na kujipatia fedha kwa njia ya udanganyifu.
Mhando alikuwa anatuhumiwa kwa matumizi mabaya ya madaraka kwa kuipa zabuni Kampuni ya Santa Clara Supplies Ltd huku akijua ana maslahi nayo na kwamba anaimiliki yeye, mke na watoto wake.
Mhando alikuwa anatuhumiwa kwa matumizi mabaya ya madaraka kwa kuipa zabuni Kampuni ya Santa Clara Supplies Ltd huku akijua ana maslahi nayo na kwamba anaimiliki yeye, mke na watoto wake.
Akisoma
hukumu hiyo, Hakimu Mkazi Hellen Riwa kwa niaba ya Hakimu mwenye kesi
hiyo Kwei Lusema amesema upande wa mashtaka umeshindwa kuthibisha juu
ya matumizi mabaya ya ofisi kwani Mhando alikuwa haingii kwenye vikao
vya maamuzi ya bodi ya Tanesco kwa hiyo alikuwa hana ushawishi wa moja
kwa moja kushawishi kampuni ya Santa Clara ambayo ni ya mke wake ipatiwe tenda
Download Video and Put Comment
Toa Maoni Hapa Chini