Jeshi
la Polisi wilayani Kahama mkoani Shinyanga limefanikiwa kuuwa Majambazi
watatu yaliokuwa yamevami duka la mtu mmoja anayejulikana kwa jina la
Emmanuel Mukumbo na kumuua kwa risasi ambapo majambazi hayo yalianza
kujibizana risasi na Polisi baada ya raia wema kuijulisha polisi na
kufika katika eneo la tukio.
Mwenyekiti wa kamati ya ulinzi na usalama wilaya ya Kahama Bw.Vita
Kawawa,amesema katika tukio hilo raia mwingine mmoja alipigwa risasi na
majambazi hao na kupoteza maisha wakati akipelekwa hospitali huku
akilipongeza jeshi la polisi kwa kazi nzuri waliyoifanya.
Akizunguymza kwa njia ya simu kaimu Kamanda wa Jeshi la Polisi
mkoani Shinyanga ACP Dismas Kisusi amethibitisha kutokea kwa tukio hilo
na kuwataka wananchi kutoa ushirikiano wa kutosha kwa jeshi la polisi
punde wanapoona dalili zozote za kiuhalifu zinafanyika.
Katika tukio hilo jeshi la polisi limefanikiwa kukamata bunduki
mbili moja aina ya Shotr Gan na moja ya kivita aina ya Uzgun,bomu la
kutupa kwa mkono, kisu cha kijeshi,risasi sitini,mkandawa kijeshi na
magazine mbili za bunduki.
Download Video and Put Comment
Toa Maoni Hapa Chini