Mwenyekiti
wa TLP taifa Dkt. Augustino Lyatonga Mrema amesisistiza ombi lake la
kazi kwa kumkumbusha Rais wa Jamhuri ya Muungano wa Tanzania Dkt. John
Pombe Magufuli kwamba ampe kazi yoyote amsaidie kibarua kigumu
alichonacho cha kuwahudumia wananchi
Dkt.
Mrema ameyasema hayo jana alipokuwa akizungumza na EATV kuhusu miaka 32
ya kifo cha aliyekuwa waziri mkuu wa Tanzania Edward Moringe Sokoine
ambaye alihudumu kwenye awamu ya kwanza ya Mwl. Julius Nyerere ambapo
alifariki akiwa na cheo cha waziri mkuu tarehe 12.04.1984 kwa ajali ya
gari.
''Namkumbuka Sokoine kama mtu wa watu aliyehudumia watu, aliyepambana na ufisadi na magendo .Alikuwa anatenda haki kwa wananchi wote .
"Hata mimi nilipokuwa waziri wa mambo ya ndani na naibu waziri mkuu nilijaribu kufanya kama yeye bahati mbaya sikufanikiwa kama yeye kwa sababu sikuwa waziri mkuu au Rais''- Alisisistiza Mrema.
"Hata mimi nilipokuwa waziri wa mambo ya ndani na naibu waziri mkuu nilijaribu kufanya kama yeye bahati mbaya sikufanikiwa kama yeye kwa sababu sikuwa waziri mkuu au Rais''- Alisisistiza Mrema.
Kuhusu Mrema kuomba kazi kwa Dkt. Magufuli
Mrema alisema kwa kutambua rekodi yake ya utendaji kazi wa Rais Dkt. Magufuli, aliwahimiza wananchi wa Vunjo wamchague kipindi cha kampeni na yeye akampigia kampeni na Rais akawaambia wananchi wa Vunjo kwamba Mrema akikosa ubunge atapangiwa kazi nyingine ndiyo hiyo wananchi wanaulizia.

Aidha Mrema alisema kuna maeneo ambayo yeye anafiti siyo lazima apewe madaraka makubwa
"Mimi sihitaji ukuu wa mkoa au uwaziri, anipe kazi yoyote na nikionana naye nitamkonyeza maeneo ambayo ninafiti ili nimsaidie kutumbua majipu." Alisema Mrema
"Mimi sihitaji ukuu wa mkoa au uwaziri, anipe kazi yoyote na nikionana naye nitamkonyeza maeneo ambayo ninafiti ili nimsaidie kutumbua majipu." Alisema Mrema
Hata hivyo Dkt. Mrema alimpongeza
Dkt. Magufuli kwamba ni mtendaji ambaye ameamua bila kusukumwa
kupambana na mafisadi na kwamba yeye ni alfa na omega na kazi hiyo
ameonyesha kwamba atafanya vizuri kuliko Sokoine na Mrema.
Download Video and Put Comment
Toa Maoni Hapa Chini