Ofisi
ya Makamu wa Rais yakanusha taarifa zinazosambazwa kwenye mitandao ya
kijamii kwamba Makamu wa Rais Samia Suluhu Hassan ameyataka makampuni ya
simu za mkononi kuzima data zao kila siku kuanzia saa 2.30 asubuhi
mpaka saa 10.30 jioni ili kuzuia Watanzania kuwa online kipindi cha muda
wa kazi na masomo kwa wanafunzi.Taarifa hizo hazina ukweli wo wote.
Makamu wa Rais hahusiki na wala hajawahi kutoa agizo hilo.Ofisi
inapenda kuujulisha umma wa Watanzania kuwa taarifa hizo ni za uzushi na
zinapaswa kupuuzwa.
Tunatoa wito kwa Watanzania kuwafichua watu wa namna hiyo wenye
tabia ya kutoa taarifa za uongo kwa kutumia jina la kiongozi huyu, huku
vyombo vya serikali vikiendelea kuwasaka ili kuwajua na taratibu za
kisheria kuchukuliwa dhidi yao.
Wakati huo huo,Mheshimiwa Makamu wa Rais anawasihi Watanzania
kutumia muda mwingi kuchapa kazi ili kujipatia maendeleo kwenye maisha
yao na siyo kutumia muda mwingi kufanya shughuli ambazo siyo za
maendeleo kwa maisha yao binafsi.
Download Video and Put Comment
Toa Maoni Hapa Chini