Kamanda wa Polisi mkoa wa Kigoma Kamishna Msaidizi Mwandamizi wa
Polisi Ferdinand Mtui amemtaja mganga huyo kuwa ni Ibrahim Bundala
(29)na kwamba anatuhumiwa kumbaka binti mwenye umri wa miaka 14
aliyefika katika zahanati hiyo kwa ajili ya kupata matibabu.
Amesema mtuhumiwa huyo ambaye atafikishwa mahakamani baada ya
uchunguzi kukamilika alitenda kosa hilo baada ya binti huyo kuingia
katika chumba cha daktari kwa ajili ya kumueleza ugonjwa anaoumwa.
Katika tukio jingine wahamiaji 55 toka Burundi wamekamatwa katika
maeneo mbalimbali baada ya kuingia nchini kinyume cha sheria na
wamekabidhiwa idara ya uhamiaji kwa ajili ya taratibu nyingine ikiwa ni
pamoja na kuwafikisha mahakamani.
Download Video and Put Comment
Toa Maoni Hapa Chini