Wilaya
ya Meatu mkoani Simiyu imebaini watumishi hewa 15 akiwemo mwalimu
aliyefariki tangu mwaka 2012 huku akiwa anaeendelea kulipwa mshahara
kiasi cha shilingi milion 21 hadi ilipogundulika juzi,baada ya kadi yake
ya benki kumezwa na mtambo wa kutolea pesa.
Akizungumza na waandishi wa habari,Mkuu wa Wilaya ya Meatu Erasto
Sima amesema kuwa baada ya zoezi la awali kukamilika la uhakiki
watumishi hewa,zoezi hilo limeendelea kuwa endelevu likifanywa katika
kata 29 ambapo wamebaini watumishi hewa 15 akiwemo mtumishi aliyefariki
zaidi ya miaka minne mshahara wake umeendelea kuchukuliwa na hivyo
meneja wa NMB tawi la Mwanhuzi kuagizwa kuizuia akaunti hiyo na pia
kumfuatilia aliyehusika na wizi huo ,huku mifumo ya mishahara ya
waliogundulika hewa imesimamishwa.
Kufuatia udanganyifu huo Mkuu huyo wa Wilaya amesema wale wote
waliobainika watafikishwa Mahakamani kwa hatua za kisheria na kuwataka
watumishi wengine ambao hawajafika katika kufanyiwa zoezi la uhakiki
katika maeneo ya kazi huku wakiendelea kuchukuwa mishahara na kwamba
iwapo nao watabainika hawataachwa.
Aidha Bw.Sima amewataka wanaoendelea na uhakiki kuwa makini na
kutolindana ili kuwaondoa wote waliohusika na udanganyifu huo kwani
zoezi hilo ni agizo la rais na linalenga kuwabaini watumishi waliokuwa
wakiibia serikali kwa muda mrefu
Download Video and Put Comment
Toa Maoni Hapa Chini