Kocha wa Barcelona Luis Enrique amesema kuwa kikosi chake
hakikuwa na pakutokea siku ya jana kutokana na kudhibitiwa vilivyo
kwenye mkondo wa pili wa robo fainali ya Klabu Bingwa Ulaya.
Barca walikiona cha mtema kuni baada ya kufungwa magoli 2-0 na wababe wa uhispania Atletico Madrid.
Kocha huyo amesema kuwa anastahili lawama kwa asilimia 99.9 kutokana na kukosa ubora siku ya jana.
Antoine Griezmann ndiye aliyeharibu kabisa usiku wa Barcelona siku ya jana huku Lionel Messi akishindwa kufunga kwenye mechi ya nne mfululizo akihaha kutafuta goli lake la 500.
Hii ni mara ya 3 kwenye miaka 11 Barcelona haijaingia nusu fainali ya mitanange hiyo.
Barca ambayo kwenye msimamo wa ligi ya uhispania ipo mbele kwa pointi 3 pekee dhidi ya Atletico imepoteza mechi nne kwenye michuano yote.
Kocha huyo wa Barcelona anasema kuwa kwa sasa wanatuliza kichwa kwani kuna makombe mengine mawili ya kupigania zaidi ikiwania La Liga na Copa Del Rey.

Kocha wa Barcelona Luis Enrique
Download Video and Put Comment
Toa Maoni Hapa Chini